Rais Luis Alberto Arce Catacora sambamba na kulaani kuendelea mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza ametangaza kuunga mkono mapambano ya wananchi wa Palestina kurejesha ardhi yao zilizoporwa na Wazayuni maghasibu.
Rais wa Bolivia aidha ameeleza kuwa, kuendelea kukandamizwa taifa la Palestina na utawala wa Kizayuni ni jambo lisilokubalika na akasema Bolivia inafanya kazi kwa ushirikiano wa nchi kadhaa ili kuhitimisha vita vya utawala huo ghasibu dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Kadhalika Rais wa Bolivia ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kufanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa, mauaji ya kimbari ya utawala ghasibuu wa Israel dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina yanafikia tamati.Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza, idadi ya Wapalestina waliouwa shahidi hadi hivi sasa tangu jeshi la Israel lianzishe mashambulizi ya kila upande Gaza mnamo tarehe 7 Oktoba 2023 ni watu 38,000 huku zaidi ya 87,000 wakijeruhiwa. Hii ni katika hali ambayo, jarida mashuhuri la masuala ya tiba na afya la The Lancet la Uingereza limeripoti kuwa, yumkini idadi halisi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza inazidi watu 186,000.
342/